Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 25

Az-Zukhruf 43:25

الزخرف

فَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُكَذِّبِينَ

Maana

Kwa hivyo, tukawalipizia. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha! [25]

[25] Basi tukawatesa walio wakadhibisha Mitume wao kwa mateso makali katika dunia. Basi hebu angalia, ewe mwenye kuzingatia, vipi ulikuwa mwisho wa wenye kukukadhibisheni kuwa ni mfano wa ajabu, na mawaidha makubwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi tukawalipizia hao (ummah) waliowakanusha Mitume wao kwa kuwateremshia mateso ya kuwadidimiza, kuwazamisha na mengineyo. Basi angalia, ulikuwa vipi mwisho wa mambo yao walipozikanusha hoja za Allah Mtukufu na mitume wake? Basi na wajihadhari watu wako wasiendelee kwenye ukanushaji wao ili yasiwapate wao yale yaliyowapata wale.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net