Az-Zukhruf 43:24
الزخرفقَـٰلَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ ءَابَآءَكُمْ ۖ قَالُوٓا۟ إِنَّا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ كَـٰفِرُونَ
Akasema (Mwonyaji): 'Hata nikiwaletea yenye uwongofu bora kuliko mliowakuta nao baba zenu?' Wakasema: 'Sisi tunayakataa tu hayo mliyotumwa nayo.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa. [24]
[24] Mwonyaji akasema: Je! Mnafuata baba zenu hata nikikujieni na yaliyo elekea zaidi kukupelekeni kwenye uwongofu kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema kuwajibu Mitume wao wakiwakadhibisha kwa Dini: Sisi tunayakataa yote mliyo tumwa kutuambia!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Huyo Muonyaji, akiwa ni Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wale Mitume waliomtangulia, huwa akisema kuwaambia waliompinga wakitumia udanganyifu huu uliotenguka, «Je, mtawafuata baba zenu, hata kama mimi nimewajia kutoka kwa Mola wenu na kitu chenye kuongoza zaidi kwenye njia ya haki, na chenye kuonyesha zaidi njia ya uongofu kuliko kile mlichowakuta baba zenu wakikifuata cha dini na mila?” Na wao huwa wakisema kwa ushindani, ”Sisi ni wenye kuyapinga na kuyakanusha hayo mliyotumwa nayo”»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net