Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 23

Az-Zukhruf 43:23

الزخرف

وَكَذَٰلِكَ مَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِى قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَآ إِنَّا وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا عَلَىٰٓ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم مُّقْتَدُونَ

Maana

Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. [23]

[23] Mfano wa hali ya watu hawa ni mfano wa mataifa yaliyo tangulia. Hatukumtuma Mtume yeyote kwenye mji kabla yako ila walisema wale wenye kuneemeka katika huo mji, nao ndio walio takabari kwa hizo neema: Hakika sisi tumewakuta baba zetu wakifuata dini hii, basi ndio sisi tunakwenda mwendo wao. Basi kufuata kijinga ni upotovu wa tangu kale.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hivyo ndivyo ilivyo, hatukutuma kabla yako, ewe Mtume, muonyaji yoyote kwenye kijiji chochote, mwenye kuwaonya na adhabu yetu kwa kutukanusha, na akawaonya na kuwatahadharisha na adhabu yetu, isipokuwa wale ambao ziliwatia kiburi neema miongoni mwa viongozi, na wakubwa huwa wakisema, ”Sisi tuliwakuta baba zetu kwenye mila na dini, na sisi ni wenye kufuata mwenendo wao na njia yao.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net