Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 7

Ash-Shura 42:7

الشورى

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ قُرْءَانًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ ٱلْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنذِرَ يَوْمَ ٱلْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ فَرِيقٌ فِى ٱلْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِى ٱلسَّعِيرِ

Maana

Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Bustanini na kundi jengine katika Moto wenye mwako mkali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni. [7]

[7] Na mfano wa ufunuo huo ulio wazi, tumekufunulia wewe hii Qur'ani kwa lugha ya Kiarabu isiyo na ubabaishi, ili upate kuwaonya watu wa Makka na walio pembezoni mwake katika Waarabu, na uwaonye watu adhabu ya siku watakao kusanywa khalaiki wote kwa ajili ya hisabu. Hapana shaka yoyote kuja siku hiyo. Watu siku hiyo watakuwa mafungu mawili - fungu moja litakuwa Peponi. ma kundi jengine litakuwa Motoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako, tulikuletea wahyi wa Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, ili uwaonye watu wa (Makkah) na watu wote wengine pembezoni mwake(1), na uwaonye na siku ya Mkusanyiko, nayo ni Siku ya Kiyama, ambayo kuja kwake hakuna shaka, ambapo watu Siku hiyo watakuwa mapote mawili: pote moja litakuwa Peponi, nalo ni lile la waliomuamini Allah Mtukufu na wakayafuata yale aliyokuja nayo Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na pote lingine litakuwa Motoni, nalo ni lile la waliomkanusha Allah Mtukufu na wakaenda kinyume na yale aliyokuja nayo Mtume Wake, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net