Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 6

Ash-Shura 42:6

الشورى

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ ٱللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ

Maana

Na wale waliowafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi bora juu yao. Wala wewe si wakili juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio wafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao. Wala wewe si wakili juu yao. [6]

[6] Na hao walio wafanya wengineo badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio wa kuwanusuru, Mwenyezi Mungu anaangalia hayo wayatendayo. Wala wewe hukupewa kazi hiyo ya kuwaangalia wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliowafanya wasiokuwa Allah Mtukufu kuwa ni waungu badala Yake wakawategemea na kuwaabudu, basi Allah Mtukufu Anavidhibiti vitendo vyao, ili Awalipe kwavyo Siku ya Kiyama. Na wewe hukuwakilishwa kuvidhibiti vitendo vyao. Hakika yako wewe ni muonyaji tu, hivyo basi ni juu yako kufikisha na ni juu yetu kuhesabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net