Ash-Shura 42:5
الشورىتَكَادُ ٱلسَّمَـٰوَٰتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِى ٱلْأَرْضِ ۗ أَلَآ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [5]
[5] Mbingu, juu ya ukubwa wake na kushikamana kwake, zimekaribia kupasuka kutoka huko juu kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu, na kuathirika kwa taadhima yake na utukufu wake. Na Malaika wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisilo elekea naye, na humsifu kwa analo stahiki. Na humwomba Mwenyezi Mungu awasamehe watu wa duniani. Na Yeye Subhanahu ananabihisha kwamba hakika ni Mwenyezi Mungu tu, peke yake, ndiye Mwenye maghfira ya wote, na rehema iliyo kunjufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zinakaribia mbingu kupasuka pasuka, kila moja juu ya ile inayoifuata, kutokana na ukubwa wa Allah Mtukufu Mwingi wa rehema na haiba Yake, Mwingi wa fadhila na utukufu, na hali Malaika wanamtakasia shukrani Mola wao na kumtakasa na kila sifa ambayo hanasibiani nayo, na wanamuomba Mola wao msamaha wa dhambi za waliyoko ardhini miongoni mwa wale wanaomuamini. Jueni mtanabahi kwamba Allah Mtukufu Ndiye mwingi wa kusamehe dhambi za waja Wake Waumini, na Ndiye Mwenye kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net