Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 8

Ash-Shura 42:8

الشورى

وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَلَـٰكِن يُدْخِلُ مَن يَشَآءُ فِى رَحْمَتِهِۦ ۚ وَٱلظَّـٰلِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ

Maana

Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angewafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu angeli penda ange wafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi. [8]

[8] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda kuwakusanya watu wote katika dunia wakafuata njia moja angeli wakusanya hivyo. Lakini Yeye humtia katika rehema yake amtakaye, kwa kuwa anajua kuwa hao wamekhiari uwongofu kuliko upotofu. Na wenye kujidhulumu nafsi zao kwa ukafiri hawana mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu wa kudhamini kuwalinda, wala msaidizi wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau angetaka Allah Mtukufu Kuwakusanya viumbe Wake kwenye uongofu na kuwafanya wawe kwenye mila moja iliyoongoka angefanya 1 Kwa kuwa Makkah ni kituo cha ardhi Umm al Q mtukufu kuliko miji yote, ndio ikawa miji yote imeizunguka Makkah na iko pembezoni mwake. U za ardhi pia umithibiti kwenye hadithi za Mtume(s kufasiri aya hii: 42:7. hivyo, lakini Yeye Anataka kuwatia kwenye rehema Yake Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Na wale wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kufanya ushirikina, basi hao hawatakuwa na yoyote wa kumtegemea atakayesimamia mambo yao Siku ya Kiyama, wala msaidizi atakayewanusuru kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu Aliyetukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net