Ash-Shura 42:38
الشورىوَٱلَّذِينَ ٱسْتَجَابُوا۟ لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ
Na wanaomwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulichowaruzuku wakawa wanatoa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Swala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa, [38]
[38] Na wanao uitikia wito wa Muumba wao na Mlezi wao, na wakamuamini, na wakazihifadhi Swala zao, na ukawa mwendo wao ni kushauriana katika mambo yao ili upatikane uadilifu katika jamii zao, bila ya mtu mmojapo au kikundi cha wachache kutaka kuwatumilia mabavu wenginewe, na wakawa wanatoa kwa njia za kheri kutokana na neema alizo mneemesha Mwenyezi Mungu;
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioitika mwito wa Mola wao wa kumpwekesha Yeye na kumtii, wakasimamisha Swala za faradhi kwa namna zake katika nyakati zake, na wakitaka jambo wanashauriana juu yake, na katika mali tuliyowapa wanatoa sadaka kwenye njia ya Allah Mtukufu, na wanatekeleza haki wanazofaradhishiwa kuwapatia wanaostahiki kama vile Zaka na matumizi na katika njia nyinginezo za matumizi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net