Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 37

Ash-Shura 42:37

الشورى

وَٱلَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلْإِثْمِ وَٱلْفَوَٰحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا۟ هُمْ يَغْفِرُونَ

Maana

Na wanaoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapokasirika wao husamehe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanayo yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao husamehe, [37]

[37] Na wanao jitenga mbali na kupanda madhambi makubwa makubwa aliyo yakataza Mwenyezi Mungu, na madhambi yote yaliyo zidi ubaya, na pindi wakichochewa kwa kufanyiwa mabaya katika mambo ya dunia yao, wao wenyewe wakawa mbele kuanza kusamehe ili kuleta masikilizano;

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao wanajiepusha na madhambi makubwa yaliyokatazwa na Allah Mtukufu, na kila kilichokuwa kichafu na kibaya miongoni mwa maasia, na wanapowakasirikia wale waliowakosea wanaufunika huo ubaya na kuusamehe kwa kuacha kumlipizia mkosaji, kwa kutaka malipo mema ya Allah Mtukufu Aliyetukuka na msamaha Wake. Na hii ni miongoni mwa tabia njema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net