Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 36

Ash-Shura 42:36

الشورى

فَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَىْءٍ فَمَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

Maana

Basi vyote mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu zaidi kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi vyote mlivyo pewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu kwa ajili ya walio amini, na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi, [36]

[36] Msidanganyike na starehe za dunia. Kwani enyi watu! Yote mliyo pewa, mali, wana, na vyenginevyo, ni starehe zenu za maisha ya duniani. Na aliyo yaandaa Mwenyezi Mungu katika neema za Peponi ni bora na zinadumu zaidi kwa wenye kuamini, na kumtegemea Muumba wao na Mlezi wao wa pekee;

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na chochote kile mnachopewa, enyi watu, cha mali na watoto na vinginevyo, ni starehe ya uhai wa ulimwenguni, kwa haraka sana itaondoka, na kilichoko kwa Allah Mtukufu cha starehe ya Pepo ya daima ni bora zaidi na ni chenye kusalia zaidi kwa wale wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake, na wakawa kwa Mola wao wanategemea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net