Ash-Shura 42:35
الشورىوَيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ يُجَـٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ
Na ili wajue wanaojadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahali popote pa kukimbilia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ili wajue wanao jadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahala pa kukimbilia. [35]
[35] Mwenyezi Mungu, Subhanahu, hufanya hayo ili Waumini wapate kuzingatia, na wajue wale wanao zirudi Ishara zake kwa upotovu kwamba wao wamo katika mkono wake, wala hawana pa kuikimbia adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wajue wale wanaojadili kwa batili kuhusu aya zetu zenye kutolea dalili upweke wetu, hawatakuwa na mahali pa kupita wala pa kuhamia kujiepusha na mateso ya Allah Mtukufu Atakapowatesa kwa dhambi zao na ukanushaji wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net