Ash-Shura 42:32
الشورىوَمِنْ ءَايَـٰتِهِ ٱلْجَوَارِ فِى ٱلْبَحْرِ كَٱلْأَعْلَـٰمِ
Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyokwenda na kurejea baharini kama vilima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyo kwenda na kurejea baharini kama vilima. [32]
[32] Na katika dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu, ni majahazi yaendayo katika bahari kama vilima virefu kwa ukubwa wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa alama Zake zenye kuonyesha uwezo Wake mkubwa na mamlaka Yake yenye kushinda ni majahazi makubwa kama majabali yanayotembea baharini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net