Ash-Shura 42:31
الشورىوَمَآ أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِى ٱلْأَرْضِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu. [31]
[31] Wala nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu na kumzuilia asilete masaibu duniani kuwa ni adhabu kwa ajili ya maasi yenu, na hata mkikimbia vipi. Na wala hamna asiye kuwa Mwenyezi Mungu wa kukurehemuni pindi ikikuteremkieni balaa, wala hamna wa kukunusuruni nayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hamkuwa, enyi watu, ni wenye kushindana na uwezo wa Allah Mtukufu juu yenu wala kuukwepa. Na hamna nyinyi asiyekuwa Allah Mtukufu Mtegemewa wa kusimamia mambo yenu na kuwapa manufaa, wala msaidizi wa kuwatetea msipatikane na madhara.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net