Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 30

Ash-Shura 42:30

الشورى

وَمَآ أَصَـٰبَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُوا۟ عَن كَثِيرٍ

Maana

Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi. [30]

[30] Na msiba wowote unao kusibuni mnao uchukia ni kwa sababu ya maasi yenu. Na anayo yasamehe Mwenyezi Mungu duniani au akayachukulia ahadi humo, basi Mwenyezi Mungu ni Karimu; hatokuwa tena wa kuadhibu kwa hayo Akhera. Na Kwa hivi ametakasika na dhulma, na amesifika kwa rehema kunjufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na msiba wowote uliowakumba, enyi watu, katika Dini yenu na dunia yenu, ni kwa sababu ya dhambi mlizozitenda na makosa. Na Mola wenu Anawasamehe nyinyi makosa mengi Asiwaadhibu kwa kuyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net