Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 29

Ash-Shura 42:29

الشورى

وَمِنْ ءَايَـٰتِهِۦ خَلْقُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَآبَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَآءُ قَدِيرٌ

Maana

Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama aliowaeneza ndani yake. Naye ni Mwenye uweza mkubwa wa kuwakusanya apendapo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama alio waeneza. Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo. [29]

[29] Na katika dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kuumba atakacho ni huku kuumba mbingu na ardhi kwa nidhamu iliyo pangwa; na kuumbwa vilivyo tenganishwa humo na kuenezwa wanayama wanao onekana na wengineo. Na Mwenyezi Mungu aliye hakikisha uweza wake kwa kuumba hivyo vilio tajwa ni Muweza wa kuwakusanya wote katika wakati autakao kuwafufulia kwa ajili ya malipo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa alama za kuonyesha ukubwa Wake, uwezo Wake na mamlaka Yake ni uumbaji mbingu na ardhi kwa namna ambayo hakukuwa na mfano uliotangulia, na aina mbalimbali za wanyama Alizozieneza humo. Na Yeye, kuwakusanya viumbe baada ya kufa kwao kwa kisimamo cha Kiyama, Anapotaka ni Muweza, hakuna kinachomshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net