Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 28

Ash-Shura 42:28

الشورى

وَهُوَ ٱلَّذِى يُنَزِّلُ ٱلْغَيْثَ مِنۢ بَعْدِ مَا قَنَطُوا۟ وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُۥ ۚ وَهُوَ ٱلْوَلِىُّ ٱلْحَمِيدُ

Maana

Naye ndiye anayeiteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Mlinzi, Mwenye kusifiwa sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye ndiye anaye iteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Mlinzi Mwenye kuhimidiwa. [28]

[28] Na Mwenyezi Mungu, peke yake, ndiye anaye iteremsha mvua inayo waokoa na ukame baada ya kwisha kata tamaa na kuzidi kiangazi, kuwa ni rehema kwa waja wake. Na Yeye hueneza baraka za mvua katika mimea, na miti ya matunda, na wanyama, na nyanda, na milima. Na Yeye, peke yake, ndiye Mwenye madaraka ya kuyapanga mambo yote ya waja wake, na ndiye wa kuhimidiwa kwa neema zake, na vitendo vyake vyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Peke Yake Ndiye Anayeteremsha mvua kutoka mbinguni, Akawanyeshea kwayo baada ya kukata tamaa kunyesha kwake, Akaeneza rehema zake kwa viumbe Vyake, Akawapa mvua ya kuwaenea, na Yeye Ndiye Mtegemewa, Anawasaidia waja Wake kwa hisani Yake na wema Wake, Msifiwa kwa uongozi wake na uendeshaji mambo Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net