Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 27

Ash-Shura 42:27

الشورى

وَلَوْ بَسَطَ ٱللَّهُ ٱلرِّزْقَ لِعِبَادِهِۦ لَبَغَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَـٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَآءُ ۚ إِنَّهُۥ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرٌۢ بَصِيرٌ

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelipanda kiburi katika dunia. Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangeli panda kiburi katika dunia. Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona. [27]

[27] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia waja wake wote, kama watakavyo, basi bila ya shaka wangeli panda kiburi katika ardhi wakafanya dhulma. Lakini Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humdhikisha amtakaye, kwa mujibu wa hikima yake. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema mambo yote ya waja wake, ya siri na dhaahiri. Basi Yeye humkadiria kila mmoja kwa linalo msilihi kwa mujibu wa hikima yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Allah Mtukufu angewakunjulia riziki waja Wake Akawapa kwa wingi, wangevuka mipaka katika ardhi kwa kiburi na ujeuri na wangetoka baadhi yao kuwadhulumu wengine. Lakini Allah Mtukufu anawateremshia riziki zao kwa kadiri atakayo ya kuwatosha. Hakika Yeye kwa waja Wake ni mtambuzi kwa yale yanayowafaa, Anaiona mipango yao na mabadiliko ya hali zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net