Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 26

Ash-Shura 42:26

الشورى

وَيَسْتَجِيبُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِۦ ۚ وَٱلْكَـٰفِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ

Maana

Na anawaitikia wanaoamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anawaitikia wanao amini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu chungu. [26]

[26] Na huwaitikia Waumini kwa wanayo yaomba, na huwazidishia juu ya hayo wanayo yaomba. Na makafiri watapata adhabu yenye kufikia ukomo wa ukali na uchungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wanamuitika Mola wao kwa kile Alichowaitia na wanajisalimisha Kwake, na Yeye Anawaongezea fadhila Zake kwa kuwaongoza na kuwazidishia malipo na thawabu. Na wale wenye kumkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake watapata adhabu kali yenye kuumiza na yenye uchungu Siku ya Kiyama .

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net