Ash-Shura 42:25
الشورىوَهُوَ ٱلَّذِى يَقْبَلُ ٱلتَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِۦ وَيَعْفُوا۟ عَنِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ
Naye ndiye anayepokea toba kwa waja wake, na anasamehe mabaya, na anayajua mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua mnayo yatenda. [25]
[25] Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kupokea toba kwa watu wanao mt'ii hata kwa makosa yaliyo zaidi kuliko yale wanayo ombea toba. Na Yeye ndiye anaye samehe madhambi yote isipo kuwa shirki, kwa kufadhili na kurehemu; na anayajua myatendayo ikiwa ya kheri au shari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Anayekubali toba kutoka kwa waja Wake wanaporudi kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtii, Ndiye Anayesamehe makosa na Ndiye Anayejua mnayoyafanya ya kheri na shari, hakuna chochote kinachofichika Kwake, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net