Ash-Shura 42:24
الشورىأَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا ۖ فَإِن يَشَإِ ٱللَّهُ يَخْتِمْ عَلَىٰ قَلْبِكَ ۗ وَيَمْحُ ٱللَّهُ ٱلْبَـٰطِلَ وَيُحِقُّ ٱلْحَقَّ بِكَلِمَـٰتِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Ati wanasema Amemzulia Mwenyezi Mungu uongo? Mwenyezi Mungu akipenda ataziba moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotovu na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ati wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga muhuri juu ya moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotofu na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliomo vifuani. [24]
[24] Je! makafiri wanasema Muhammad anamzulia uwongo Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu akipenda atakufungia moyo wako usubiri maudhi yao, na tuhuma yao kuwa unamzulia Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ataondoa na ataushinda ukafiri na ataupa nguvu Uislamu na ataudhihirisha kwa wa'hyi alio mteremshia Mtume wake s.a.w., kwani - Yeye- Mwenyezi Mungu anajua yote yaliomo ndani ya nyoyo zenu nyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au je, wanasema hawa washirikina, kwamba Muhammad amemzushia Allah Mtukufu urongo ndipo akaja na hiki anachokisoma kwa kukizua mwenyewe? Basi Allah Mtukufu Ataupiga mhuri moyo wako, ewe Mtume, uwapo utafanya hivyo. Na Allah Mtukufu Anaiondoa batili na kuifuta, na Anaithibitisha haki kwa maneno Yake, ambayo hayabadiliki wala hayageuki, na kwa ahadi Yake ya kweli isiyoenda kinyume. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi sana wa yaliyomo ndani ya nyoyo za waja, hakuna chochote kinachofichika kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net