Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 23

Ash-Shura 42:23

الشورى

ذَٰلِكَ ٱلَّذِى يُبَشِّرُ ٱللَّهُ عِبَادَهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ ۗ قُل لَّآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا ٱلْمَوَدَّةَ فِى ٱلْقُرْبَىٰ ۗ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُۥ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ شَكُورٌ

Maana

Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema. Sema: 'Sikuombeni malipo yoyote juu yake ila mapenzi katika kujikurubisha. Na anayefanya wema, tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu mno, Mwenye shukrani sana.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ndiyo aliyo wabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walio amini na wakatenda mema. Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha. Na anaye fanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye shukrani. [23]

[23] Hiyo fadhila kubwa ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu amewabashiria waja wake Waumini, wat'iifu. Ewe Mtume! Sema: Mimi sitaki kwenu ujira kwa kufikisha huu Ujumbe, isipo kuwa mumpende Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika kujikurubisha kwenu kwake Yeye Subhanahu, kwa vitendo vyema. Na mwenye kutenda ut'iifu Mwenyezi Mungu atampa ujira mara mbili. Hakika Mwenyezi Mungu ni mkunjufu wa maghfira kwa wenye madhambi, ni Mwenye shukrani kwa waja wake wenye vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo ambayo niliwapa habari kwayo, enyi watu, miongoni mwa starehe na matukufu ya Akhera ndio yale ambayo Allah Mtukufu Anawapa bishara kwayo waja Wake wema waliomuamini na kumtii duniani. Sema, ewe Mtume, uwaambie wale wanaofanya shaka kuhusu Kiyama miongoni mwa washirikina wa watu wako, «Siwaombi kwa huu ulinganizi wangu wa haki niliokuja nao mnipe malipo kwenye mali zenu, isipokuwa mnitekelezee haki yangu ya ujamaa kwenu na muunge udugu ulioko baina yangu mimi na nyinyi.» Na yoyote mwenye kutenda jema tutamuongezea mara kumi na zaidi. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kusamehe kwa wingi dhambi za waja Wake, ni Mwingi wa shukrani kwa mema yao na utiifu wao Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net