Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 22

Ash-Shura 42:22

الشورى

تَرَى ٱلظَّـٰلِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا۟ وَهُوَ وَاقِعٌۢ بِهِمْ ۗ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فِى رَوْضَاتِ ٱلْجَنَّاتِ ۖ لَهُم مَّا يَشَآءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْكَبِيرُ

Maana

Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na wale walioamini na wakatenda mema watakuwemo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao Mlezi. Hiyo ndiyo fadhila kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Utawaona hao madhaalimu wanavyo kuwa na khofu kwa sababu ya waliyo yachuma, nayo yatawafika tu. Na walio amini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao Mlezi. Hiyo ndiyo fadhila kubwa. [22]

[22] Ewe unaye semezwa! Utawaona Siku ya Kiyama hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ushirikina wamo katika khofu kuogopa malipo ya ushirikina wao, nayo yatawateremkia tu hapana hivi wala hivi. Na utawaona wenye kuamini na wakatenda mema wamestarehe katika mwahali mzuri kabisa katika Pepo. Humo watapata neema wazitamaniazo kwa Mola wao Mlezi. Hayo ndiyo malipo makubwa, na ndio fadhila kubwa ya kutarajiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Utawaona, ewe Mtume, makafiri Siku ya Kiyama wako katika hali ya kuogopa mateso ya Allah Mtukufu kwa yale matendo mabaya waliyoyatenda duniani, na adhabu itawashukia, na wao hapana budi wataionja. Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na wakamtii, wataingia kwenye mabustani ya Pepo na majumba yake na starehe za Akhera, na watakuwa na kila kinachotamaniwa na nafsi zao kwa Mola wao. Hayo Aliyowapa Allah Mtukufu ya fadhila na utukufu ndiyo nyongeza isiyosifika na isiyofikiwa na akili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net