Ash-Shura 42:21
الشورىأَمْ لَهُمْ شُرَكَـٰٓؤُا۟ شَرَعُوا۟ لَهُم مِّنَ ٱلدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَنۢ بِهِ ٱللَّهُ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةُ ٱلْفَصْلِ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ ۗ وَإِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisingekuweko neno la kupambanua, basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyo itolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisinge kuwako neno la kupambanua basi wangeli katiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu. [21]
[21] Kwani wao wanao miungu walio watungia dini nyengine asiyo iamrisha Mwenyezi Mungu? Hayakuwa hayo! Na lau halikwisha tangulia agano la kuakhirisha hukumu mpaka Siku ya Kiyama, basi bila ya shaka pangeli hukumiwa baina ya makafiri na Waumini hapa hapa duniani. Na hakika walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri watapata adhabu yenye machungu makali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, kwani hawa wenye kumshirikisha Allah Mtukufu wana washirika katika ushirikina wao na upotevu wao waliowazushia katika dini kitu Asichoamuru Allah Mtukufu? Na lau si hukumu ya Allah Mtukufu na makadirio Yake ya kuwapa muhula na kutowaharakishia adhabu duniani, wangehukumiwa kuharakishiwa adhabu. Na kwa hakika wale wenye kumkanusha Allah Mtukufu watakuwa na adhabu yenye uchungu na kuumiza Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net