Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 33

Ash-Shura 42:33

الشورى

إِن يَشَأْ يُسْكِنِ ٱلرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِۦٓ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ

Maana

Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye subira kubwa na akashukuru sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru. [33]

[33] Mwenyezi Mungu akipenda huutuliza upepo kukawa shuwari; basi majahazi yaliyo thibiti juu ya bahari hutulia hayendi huko yendako. Hakika huko kwenda kwao na kusimama kwao kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni dalili wazi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu. Wanayazingatia hayo Waumini wenye kusubiri wakati wa dhiki, na wenye kushukuru wakati wa furaha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Anapotaka Allah Mtukufu Anautuliza upepo, na majahazi yanakua ni yenye kutulia juu ya mgongo wa bahari na kutotembea. Hakika katika kutembea majahazi haya na kusimama kwake baharini kwa uwezo wa Allah Mtukufu pana mawaidha na hoja za wazi za uwezo wa Allah Mtukufu, kwa kila mwingi wa uvumilivu juu ya kumtii Allah Mtukufu, kujiepusha na vitendo vya kumuasi na kukubali makadirio Yake, mwingi wa shukrani wa neema Zake na mema Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net