Ash-Shura 42:11
الشورىفَاطِرُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا وَمِنَ ٱلْأَنْعَـٰمِ أَزْوَٰجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚ لَيْسَ كَمِثْلِهِۦ شَىْءٌ ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi. Amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama wa kufugwa waliwao dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. [11]
[11] Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuumbieni katika jinsi yenu wanaume na wanawake, na akaumba katika mifugo yenu kadhaalika madume na majike, na kwa mpango huu ndio wazidi kuwa wengi. Hapana kitu chochote kama mfano wake Mwenyezi Mungu, basi hana kitu cha kuwa wa pili yake. Na Yeye ndiye Mwenye kujua, kwa ujuzi wa kukamilika, kuvijua vyote vinavyo sikilizana na kuonekana bila ya taathira ya hisiya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, kutakasika ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Muumba mbingu na ardhi na Muanzilishi wa kuzitengeneza kwa uwezo Wake na matakwa Yake na hekima Yake. Amewapatia nyinyi wake wanaotokana na nyinyi ili mjitulize kwao, na Amewapatia wanyama howa wa kila aina, wa kiume na wa kike. Anawafanya muwe wengi kwa kuzaana kwa njia hii ya kutangamana. Hakuna kinachofanana naye na kuwa kama Yeye chochote kile miongoni mwa viumbe vyake, si katika dhati Yake wala majina Yake wala sifa Zake wala vitendo Vyake. Kwani majina Yake yote ni mazuri na sifa Zake ni za ukamilifu na utukufu; na kwa vitendo Vyake Amefanya vipatikane viumbe vikubwa bila ya kuwa na mshirika. Na Yeye Ndiye Mwenye kusikia na Ndiye Mwenye kuona. Hakuna chochote kinachofichika Kwake cha matendo ya waja Wake na maneno yao, na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net