Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 10

Ash-Shura 42:10

الشورى

وَمَا ٱخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَىْءٍ فَحُكْمُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبِّى عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ

Maana

Na mkihitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi ninayemtegemea, na kwake Yeye narejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye narejea. [10]

[10] Na mliyo khitalifiana kwayo katika mambo yaliyo khusu Imani na ukafiri, hukumu yake ya kukata iko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye amekwisha ibainisha. Yeye huyo ndiye Hakimu wa kuhukumu mliyo khitalifiana, Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki mambo yangu yote. Mimi namtegemea Yeye kwa mambo yangu. Na kwake Yeye peke yake ndio narejea ili kutafuta uwongozi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kitu chochote kile mnachotafautiana kwacho, enyi watu, miongoni mwa mambo ya dini yenu, basi hukumu irudishwe kwa Allah Mtukufu katika Kitabu Chake na (Sunnah) ya Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Huyo Ndiye Allah Mtukufu, Mola wangu na Mola wenu, Kwake Yeye nimetegemea katika mambo yangu, na Kwake Yeye ninarejea katika hali zangu zote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net