Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 12

Ash-Shura 42:12

الشورى

لَهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi zaidi wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. [12]

[12] Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi, kwa kuzihifadhi na kuzitumia. Humkunjulia riziki amtakaye, na humdhikisha amtakaye. Hakika Yeye, Mtukufu, ujuzi wake umezunguka kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni Wake Yeye, kutakasika ni Kwake, ufalme wa mbinguni na ardhini, na mkononi Mwake kuna funguo za rehema na riziki, Anamkunjulia riziki Yake Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na anampunguzia Anayemtaka. Hakika Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, ni Mjuzi wa kila kitu, Hakifichiki Kwake chochote katika mambo ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net