Fussilat 41:7
فصلتٱلَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ كَـٰفِرُونَ
Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera. [7]
[7] Na washirikina wasio toa Zaka kuwapa wanao stahiki watapata adhabu kali. Na wao tu, si wenginewe, ndio wanao kataa kuwa upo uhai wa Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wasiojisafisha nafsi zao kwa kumpwekesha Mola wao na kumtakasa, na wasiotoa Zaka kuwapa wanaostahiki, basi hao hawamtakasii Muumba wala hawanufaishi viumbe; na wao hawaamini Ufufuzi wala Pepo na Moto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net