Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 6

Fussilat 41:6

فصلت

قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ فَٱسْتَقِيمُوٓا۟ إِلَيْهِ وَٱسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ

Maana

Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanaomshirikisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanao mshirikisha! [6]

[6] Ewe Mtume! Waambie: Hakika mimi si chochote ila ni mtu mfano wenu nyinyi, napata Wahyi (Ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwamba wa kuabudiwa kwa haki na nyinyi ni Mungu Mmoja tu. Basi fuateni Njia Iliyo Nyooka ya kwendea kwake! Na mtake kwake msamaha kwa madhambi yenu. Na washirikina wasio toa Zaka kuwapa wanao stahiki watapata adhabu kali. Na wao tu, si wenginewe, ndio wanao kataa kuwa upo uhai wa Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, (ewe Mtume), «Hakika yangu mimi ni binadamu kama nyinyi, Allah Mtukufu Ananiletea wahyi kwamba Mola wenu Anayestahiki kuabudiwa ni Mola Mmoja Asiyekuwa na mshirika. Basi fuateni njia yenye kufikisha Kwake na mtake msamaha Wake.» Maangamivu na mateso yatawapata washirikina walioabudu masanamu, yasiyonufaisha wala kudhuru, badala ya kumuabudu Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net