Fussilat 41:8
فصلتإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, watakuwa na ujira usio na ukomo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao amini na wakatenda mema watakuwa na ujira usio na ukomo. [8]
[8] Hakika Waumini wanao tenda mema watapata malipo mazuri yasiyo katika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale wanaomuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na Kitabu Chake na wakafanya matendo mema, hali ya kumtakasia Allah Mtukufu katika matendo hayo, watapata malipo makubwa yasiyokatika wala kuzuiliwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net