Fussilat 41:24
فصلتفَإِن يَصْبِرُوا۟ فَٱلنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا۟ فَمَا هُم مِّنَ ٱلْمُعْتَبِينَ
Basi wakisubiri, Moto ndio maskani yao. Na wakiomba radhi, hawakubaliwi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wakisubiri Moto ndio maskani yao. Na wakiomba radhi hawakubaliwi. [24]
[24] Basi hata wakijizuia machungu yao, Moto ndio mwisho wao, na makaazi yao ya daima. Na wakitaka kumridhi Mwenyezi Mungu sasa hawakubaliwi hayo matakwa yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakivumilia adhabu, basi Moto ndio makazi yao, na wakiomba kurejea duniani waanze kufanya amali njema huko, hawatajibiwa ombi hilo wala hazitakubaliwa nyudhuru zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net