Fussilat 41:23
فصلتوَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ ٱلَّذِى ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَىٰكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ
Basi hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi, imekuangamizeni; na mmekuwa miongoni mwa waliohasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi hiyo dhana yenu mliyo kuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi. Imekuangamizeni; na mmekuwa miongoni mwa walio khasiri. [23]
[23] Lakini dhana mbovu mliyo kuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi imekuhilikini, na kwa hivyo mmekuwa Siku ya Kiyama katika wenye kukhasiri vibaya mno.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hiyo ndiyo dhana yenu mbovu ambayo mliidhania kwa Mola wenu; imewaangamiza na kuwatia Motoni, ndipo mkawa Leo ni miongoni mwa wale waliopata hasara ya nafsi zao na watu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net