Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 22

Fussilat 41:22

فصلت

وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَآ أَبْصَـٰرُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ ٱللَّهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ

Maana

Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika yale mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyo kuwa mkiyatenda. [22]

[22] Wala nyinyi hamkuwa mkiweza kuficha vitendo vyenu viovu hata viungo vyenu visivione na ikawa macho yenu, na masikio yenu na ngozi zenu, vyote hivyo vikakushuhudilieni. Lakini nyinyi mlikuwa mkidhani kuwa Mwenyezi Mungu hajui mengi katika vitendo vyenu, kwa sababu mkivifanya kwa uficho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hamkuwa mkijificha mlipokuwa mkitenda maasia kwa kuogopa yasije masikio yenu wala macho yenu wala ngozi zenu zikatoa ushahidi dhidi yenu Siku ya Kiyama, lakini mlidhani, kwa kufanya maasia kwenu, kuwa Allah Mtukufu hajui mengi kuhusu matendo yenu ambayo kwayo mlimuasi Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net