Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 21

Fussilat 41:21

فصلت

وَقَالُوا۟ لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوٓا۟ أَنطَقَنَا ٱللَّهُ ٱلَّذِىٓ أَنطَقَ كُلَّ شَىْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Maana

Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye alitamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliye kuumbeni mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa. [21]

[21] Na hao maadui wa Mwenyezi Mungu wakaziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Na ngozi zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu aliye tamkisha kila kitu. Na Yeye ndiye aliye kuumbeni hapo mwanzo kabla hamjawa chochote. Na kwake Yeye, peke yake, ndio mtarejea baada ya kufufuliwa, akuhisabieni mliyo kwisha yatanguliza katika vitendo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na watasema hao watakaokusanywa kupelekwa Motoni miongoni mwa maadui wa Allah Mtukufu kuziambia ngozi zao wakizilaumu, «Kwa nini mmetoa ushahidi dhidi yetu?» Na hapo ngozi zao ziwajibu, «Ametutamsha Allah Mtukufu Ambaye Amekitamsha kila kitu, na Yeye Ndiye Aliyewaumba nyinyi mara ya kwanza na hamkuwa ni chochote, na kwake Yeye Ndio mwisho wenu baada ya kufa ili mhesabiwe na mlipwe».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net