Fussilat 41:25
فصلتوَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَآءَ فَزَيَّنُوا۟ لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ فِىٓ أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ خَـٰسِرِينَ
Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyo pita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kukhasirika. [25]
[25] Nasi tumewaandalia duniani marafiki waharibifu, na wao wakawazainishia mbele yao mambo ya Akhera, basi wakawaghuri kwamba ati hakuna kufufuliwa wala kuhisabiwa, na wakawapambia pia mambo ya duniani ili wastarehe nayo. Na neno la adhabu lilio wapata mataifa yaliyo kwisha pita miongoni mwa majini na watu walio kuwa kama wao, likawathibitikia na wao kwa sababu ya kukhiari kwao upotovu badala ya uwongofu. Hakika watu hao wote walikuwa katika walio khasiri khasara iliyo timia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwawekea hawa madhalimu wenye kukanusha marafiki wabaya miongoni mwa Mashetani wa kibinadamu na wa kijini, wakawapambia matendo yao machafu duniani, wakawaita kwenye ladha zake na matamanio yake ya haramu, na wakawapambia wao yaliyo nyuma yao katika mambo ya Akhera wakawasahaulisha wasiikumbuke, na wakawalingania wakatae Marejeo (ya Kiyama). Na kwa hiyo walistahili kuingia Motoni wawe miongoni mwa wale makafiri wa (ummah) waliopita wa kijini na wa kibinadamu. Wao walikuwa wamepata hasara ya matendo yao duniani na hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net