Fussilat 41:16
فصلتفَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِىٓ أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ ٱلْخِزْىِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ
Basi tukawatumia upepo wa kimbunga katika siku za misiba, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za ukorofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa. [16]
[16] Tukawapelekea upepo wenye sauti kali katika siku korofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwafanya wawe madhalili wanyonge katika maisha ya duniani. Na ninaapa kuwa bila ya shaka adhabu ya Akhera itakuwa ya hizaya zaidi, wala wao siku hiyo hawatapata wa kuwasaidia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tukawatumia wao upepo wenye ubaridi mkali, wenye sauti kubwa, katika siku zilizokuwa korofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya unyonge na udhalili katika maisha ya kilimwengu. Na adhabu ya Akhera ina unyonge na utwevu mwingi zaidi, na wao hawatasaidiwa kwa kuzuia adhabu isiwapate.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net