Fussilat 41:15
فصلتفَأَمَّا عَادٌ فَٱسْتَكْبَرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَقَالُوا۟ مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِى خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَجْحَدُونَ
Ama kina 'Adi, hao walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Ni nani mwenye nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliyewaumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu! [15]
[15] Ama kina A'di walipandwa na kiburi katika nchi bila ya haki ya kuwa na kiburi hicho. Na walisema kwa kughurika na nafsi zao: Nani huyo anaye tushinda sisi kwa nguvu? Ama ajabu watu hawa! Wanasema hayo na wao hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ana nguvu zaidi kuwashinda wao? Na wao walikuwa wakizikanya Ishara zetu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama hao (‘Ãd, watu wa Hūd), waliwafanyia watu ujeuri bila haki na wakasema kwa kujiona, «Ni nani mwenye nguvu kali zaidi kushinda sisi?» Kwani hawaoni kuwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, Aliyewaumba ni Mkali zaidi wa nguvu na kipigo? Na walikuwa ni wenye kuzikanusha hoja zetu na dalili zetu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net