Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 14

Fussilat 41:14

فصلت

إِذْ جَآءَتْهُمُ ٱلرُّسُلُ مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّا ٱللَّهَ ۖ قَالُوا۟ لَوْ شَآءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَـٰٓئِكَةً فَإِنَّا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ كَـٰفِرُونَ

Maana

Walipowajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angelitaka Mola wetu Mlezi, bila ya shaka angeliwateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walipo wajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angeli taka Mola wetu Mlezi bila ya shaka angeli wateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyo tumwa. [14]

[14] Walijiwa A'di na Thamudi na hiyo adhabu walipo watokelea Mitume pande zote. Hawakuacha njia ya kuwaongoza ila waliipitia, na wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu. Wao wakasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli taka kumtuma Mtume basi angeli tuteremshia Malaika. Basi sisi hakika tunakataa hayo ya Tawhidi na mengineyo mliyo kuja nayo nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walipowajia Mitume hao kina ‘Ãd na Thamûd, wao baada ya wengine wakifuatana, wakiwaamrisha kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake Asiyekuwa na mshirika, waliwaambia Mitume wao, «Lau Allah Mtukufu angetaka tumpwekeshe na tusiabudu chochote kisichokuwa Yeye, Angeteremsha Malaika kutoka mbinguni wakiwa wajumbe wa hilo unalotuitia kwalo, na asingewatuma nyinyi na hali nyinyi ni binadamu kama sisi, basi sisi kwa lile ambalo Allah Mtukufu Amewatuma kwetu la kumuamini Allah Mtukufu Peke Yake ni wenye kulikanusha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net