Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 13

Fussilat 41:13

فصلت

فَإِنْ أَعْرَضُوا۟ فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَـٰعِقَةً مِّثْلَ صَـٰعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ

Maana

Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya 'Adi na Thamudi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A'di na Thamudi, [13]

[13] Basi washirikina wakipuuza Imani baada ya kuwekewa wazi dalili zake, wewe, Mtume, waambie: Nimekuonyeni msije kupatilizwa kwa adhabu kali kama iliyo wateketeza kina A'di na Thamudi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi wakipuuza wakanushaji hawa baada ya kubainishiwa sifa za Qur’ani zinazotajika vyema, na sifa za Mungu Mkubwa, waambie, «Kwa kweli, ninawaonya nyinyi na adhabu yenye kuwamaliza mfano wa adhabu iliyowashukia watu wa kabila la ‘Ãd na Thamûd walipomkanusha Mola wao na kuwaasi Mitume wao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net