Fussilat 41:17
فصلتوَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَـٰهُمْ فَٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْعَمَىٰ عَلَى ٱلْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَـٰعِقَةُ ٱلْعَذَابِ ٱلْهُونِ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Na ama Thamudi, hao tuliwaongoza, lakini walipendelea upofu kuliko uongofu. Basi ukawachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehesha kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walipenda upofu kuliko uwongofu. Basi uliwachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma. [17]
[17] Na ama kina Thamudi tuliwabainishia njia ya kheri na njia ya shari. Lakini wao walikhiari upotovu kuliko uwongofu, ikawatwaa radi iliyo waunguza kwa madhila na unyonge, kwa sababu ya madhambi waliyo yachuma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ama hao Thamûd, (watu wa Ṣāliḥ), kwa hakika tuliwabainishia njia ya uongofu na usawa, wakafadhilisha upofu juu ya uongofu, kikawaangamiza wao kimondo cha adhabu yenye kutweza, kwa sababu ya dhambi waliokuwa wakizitenda, kwa kumkufuru kwao Allah Mtukufu na kuwakanusha Mitume Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net