Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 91

An-Nisaa 4:91

النساء

سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا۟ قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوٓا۟ إِلَى ٱلْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا۟ فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوٓا۟ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓا۟ أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَـٰنًا مُّبِينًا

Maana

Mtawakuta wengine wanataka wapate salama kwenu na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitina, hudidimizwa humo. Na ikiwa hawajitengi nanyi, na wakawaletea salama, na wakaizuia mikono yao, basi wakamateni na waueni popote mnapowakuta. Na hao, tumewapa nyinyi hoja zilizo wazi juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mtawakuta wengine wanataka wapate salama kwenu na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitna hudidimizwa humo. Ikiwa hawajitengi nanyi, na wakakuleteeni salama, na wakazuia mikono yao, basi wakamateni na wauweni popote mnapo wakuta. Na juu ya hao ndio tumekupeni hoja zilizo wazi. [91]

[91] Mkiwashinda washirikina, hao wanaafiki huwa pamoja nanyi; na washirikina wakiwashinda Waislamu, wao huwa pamoja na washirikina. Wao hutaka wapate amani kwa Waislamu na wapate amani kwa jamaa zao washirikina. Hawa wamo katika upotovu na unaafiki wa moja kwa moja. Ikiwa hawatoacha kukupigeni vita na wakakutangazieni amani na salama, basi wauweni popote muwapatapo. Kwani kwa kuto kujitenga na kukupigeni vita, basi inakuwa Waumini wana haki kuwauwa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa Waumini hoja iliyo wazi kuwapiga vita.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mtawapata watu wengine miongoni mwa wanafiki wanapenda kuzituliza nafsi zao upande wenu kwa kuwaonyesha kuwa wana Imani na pia wanapenda kujituliza upande wa watu wao walio makafiri kwa kuwaonyesha kuwa wao wako kwenye ukafiri. Kila wakirudishwa kwenye mahali pa ukafiri na makafiri, huingia kwenye hali mbaya zaidi. Basi hawa wasipojiepusha na nyinyi, wakajisalimisha kwenu kikamilifu na wakajizuia wasipigane na nyinyi, washikeni kwa nguvu na muwaue popote waliopo. Wale ndio ambao waliofikia, katika njia hii mbaya sana, kiasi cha kuwapambanua wao na wasiokuwa wao; wao ndio ambao tumewapa nyinyi hoja iliyo wazi ya kuwaua na kuwateka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net