Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 73

An-Nisaa 4:73

النساء

وَلَئِنْ أَصَـٰبَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُنۢ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُۥ مَوَدَّةٌ يَـٰلَيْتَنِى كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا

Maana

Na ikikupateni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, anasema, kana kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu na yeye: 'Aa! Laiti ningelikuwa pamoja nao nikafuzu kufuzu kukubwa.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikIkufikieni Fadhila kutoka kwa Mwenezi Mungu husema, kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu naye, laiti ni ngekuwa baina yao nikafanikiwa Mafanikio makubwa [73]

[73] Na mnapo pata fadhila ya ushindi kutokana na Mwenyezi Mungu, mkapata ngawira za vita, kikundi hicho hicho, kwa kuona maya na kutamani, husema: Laiti tungeli kuwa nao katika vita hivi, nasi tukapata mafanikio ya ngawira nzuri. Na husema haya na hayo kama kwamba hapakuwepo mapenzi yoyote yaliyo wafunga wao na nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na itokeapo mkapata fadhila za Mola wenu na ngawira, wao wanasema, kwa uhasidi na majuto, kama kwamba hakukuwa na mapenzi ya waziwazi baina yenu, «Laiti mimi ningekuwa pamoja na wao nikafaulu kupata yale waliyoyapata: ya kuokoka, ushindi na ngawira».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net