An-Nisaa 4:74
النساءفَلْيُقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يَشْرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا بِٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا
Basi na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanauza uhai wa dunia kwa Akhera. Na mwenye kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha akauwawa au akashinda, basi tutampa ujira mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa. [74]
[74] Ikiwa yupo kati yenu anaye bakia nyuma asende kupigana kutokana na udhaifu wa Imani yake, au ulegevu wa azma yake, basi na wapigane, kuinua Neno la Mwenyezi Mungu na kuwania Haki, wale walio uza uhai wao wa dunia kutafuta uhai wa Akhera. Na mwenye kupigana vita kwa ajili ya kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kuwania Haki, atapata moja ya mema mawili. Ama atauliwa apate fadhila ya kufa shahidi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au atashinda, apate fadhila ya kufuzu katika dunia. Naye katika hali zote mbili atapewa na Mwenyezi Mungu ujira mkubwa katika Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi na wapigane jihadi, katika njia ya kuinusuru dini ya Allah Mtukufu na kulitukuza neno Lake, wale wanaouza uhai wa dunia kwa Akhera na thawabu zake. Na yoyote mwenye kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu kidhati, akauawa au akashinda, basi tutampa malipo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net