An-Nisaa 4:72
النساءوَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَـٰبَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَىَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا
Na hakika yupo kati yenu anayejikokota sana. Na ukikupateni msiba, husema: 'Hakika Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa vile sikuwa nimehudhuria pamoja nao.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na yupo kati yenu anaye bakia nyuma; na ukikusibuni msiba husema: Mwenyezi Mungu kanifanyia kheri sikuwa nao. [72]
[72] Na wahadharisheni wanao kaa nyuma wasende nanyi vitani. Miongoni mwa hao mnao ishi nao wakajizuia wasifuatane nanyi kwenda kupigana, mkipatwa na shida na masaibu katika Jihadi, wao wa kikundi hicho, kwa kufurahia yaliyo kusibuni, husema: Mwenyezi Mungu katufanyia kheri kwa kuwa hatukwenda nao vitani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika miongoni mwenu kuna watu wenye kujichelewesha kutoka kuenda kupambana na maadui kwa kuona uzito kufanya hivyo, na kufanya bidii kuwavunja moyo wengine kwa kusudi. Itokeapo mkapatikana kuuawa na kushindwa, huwa wakisema kwa furaha, «Allah Mtukufu Ametulinda kwa kutokuwako na wale waliopatikana na mambo ambayo nafsi zetu zinayachukia.» Na hilo la kutokuwa na nyinyi huwa likiwafurahisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net