Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 175

An-Nisaa 4:175

النساء

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَٱعْتَصَمُوا۟ بِهِۦ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِى رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَٰطًا مُّسْتَقِيمًا

Maana

Ama wale waliomwamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawaingiza katika rehema itokayo kwake, na fadhila, na atawaongoa kwenye Njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [175]

[175] Ama walio msadiki Mwenyezi Mungu na ujumbe wake alio leta, na wakaifuata Dini yake, atawatia katika Bustani zake Akhera, na atawamiminia rehema yake, na atawakusanya katika ukunjufu wa fadhila yake, na atawawezesha hapa duniani kuthibiti katika Njia yake Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ama wale waliomuamini Allah Mtukufu kiitikadi, kimaneno na kivitendo, na wakashikamana na Nuru ambayo waliteremshiwa, Atawaingiza Peponi ikiwa ni rehema na fadhila kutoka Kwake na Atawaafikia kufuata njia iliolingana sawa, itakayopelekea kwenye mabustani ya Peponi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net