Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 174

An-Nisaa 4:174

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُم بُرْهَـٰنٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا

Maana

Enyi watu! Hakika umekwishawafikia ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na tumewateremshia nuru iliyo wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi. [174]

[174] Enyi watu wote! Zimekwisha kujieni dalili zilizo wazi za ukweli wa Mtume Muhammad. Na tumekuteremshieni kwa ulimi wake Qur'ani iliyo wazi kama mwangaza, unao angaza Njia, na inayo kuongozeni kwendea mafanikio.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu, kwa hakika umekuja kwenu ushahidi kutoka kwa Mola wenu, nao ni Mtume wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo miongoni mwa maelezo yaliyo waziwazi na hoja za yakini, kubwa ya hizo ni Qur’ani tukufu, zenye kutolea ushahidi ukweli wa unabii wake na utume wake wa mwisho; na tumewateremshia Qur’ani ikiwa ni uongofu na ni nuru yenye kufafanua mambo waziwazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net