Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 172

An-Nisaa 4:172

النساء

لَّن يَسْتَنكِفَ ٱلْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّهِ وَلَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ٱلْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا

Maana

Masihi hatajiinua juu zaidi kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika waliowekwa karibu. Na mwenye kujiinua juu zaidi ya kumuabudu Yeye Mwenyezi Mungu na akafanya kiburi, basi atawakusanya wote kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Masihi hataona uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika walio karibishwa. Na watakao ona uvunjifu utumwa wa Mwenyezi Mungu na kufanya kiburi, basi atawakusanya wote kwake. [172]

[172] Masihi hakujiona bora hata akatae kuwa ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala hawakujiona bora Malaika walio karibishwa. Na mwenye kutakabari na kujiona mtu wa juu hataweza kuikimbia adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku atakayo wakusanya watu kwa ajili ya hisabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hatakataa Al-Masîḥ kuwa ni mja wa Allah Mtukufu. Vilevile hawatakataa Malaika waliokaribishwa kuwa wao ni waja wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Na yoyote mwenye kukataa kufuata kikamilifu na kunyenyekea na akafanya kiburi, Basi hao Allah Mtukufu Atawafufua Awakusanye Kwake Siku ya Kiyama, Atoe uamuzi baina yao kwa hukumu Yake ya uadilifu na Amlipe kila mmoja kwa kile anachostahili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net