Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 163

An-Nisaa 4:163

النساء

إِنَّآ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ كَمَآ أَوْحَيْنَآ إِلَىٰ نُوحٍ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعْدِهِۦ ۚ وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَـٰرُونَ وَسُلَيْمَـٰنَ ۚ وَءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ زَبُورًا

Maana

Hakika Sisi tumekufunulia ufunuo (wahyi) wewe kama tulivyomfunulia ufunuo (wahyi) Nuhu na Manabii waliokuwa baada yake. Na tulimfunulia ufunuo (wahyi) Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wanawe, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, naye Daud tukampa Zaburi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. [163]

[163] Hakika Sisi tumekufunulia wewe, ewe Nabii! (tumekuteremshia Wahyi), Qur'ani na Sharia, kama tulivyo wafunulia kabla yako Nuhu na Manabii wa baada yake, na kama tulivyo wapa Wahyi Ibrahim, na Ismail, na Is-haq, na Yaakub, na wajukuu zake, nao wale walio kuwa Manabii wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa dhuriya (wazao) wa Yaakub, na Isa, na Ayubu, na Yunus, na Haarun, na Suleiman, na kama tulivyo mfunulia Daud tukamteremshia Kitabu cha Zabur.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika sisi tumekuletea wahyi, ewe Mtume, ili ufikishe ujumbe kama tulivyomletea wahyi Nûḥ na Manabii wengine baada yake. Na tumewapelekea wahyi Ibrãhîm, Ismã‘îl, Isḥãq, Ya‘qûb na Asbãṭ, nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya wana wa Isrãîl wanaotokana na kizazi cha Ya‘qûb, na pia ‘Ǐsâ, Ayyûb, Yûnus, Hãrûn na Sulaimãn na tukampa Dãwûd Zaburi, nacho ni kitabu na kurasa zilizoandikwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net