Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 164

An-Nisaa 4:164

النساء

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَـٰهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

Maana

Na Mitume tuliokwishakukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine ambao hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alizungumza na Musa kwa maneno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno. [164]

[164] Kadhaalika tumewatuma Mitume wengi ambao tumekwisha taja khabari zao kabla yake. Na Mitume wengine hatukukusimulia hadithi zao. Na njia ya kumpa Wahyi Musa ilikuwa Mwenyezi Mungu akisema naye moja kwa moja nyuma ya pazia, lakini bila ya kuwepo mwengine kati.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tumewatumiliza Mitume ambao tumekuelezea habari zao katika Qur’ani, kabla ya aya hii, na Mitume wengine ambao hatukukuelezea habari zao kwa hekima tuliyoikusudia.Na Allah Mtukufu Alisema na Mûsã waziwazi ili kumtukuza kwa sifa hii. Katika aya hii tukufu kuna uthibitisho wa sifa ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ya kusema kama inavyolingana na utukufu Wake, na kwamba Yeye Allah Mtukufu Alisema na Nabii Wake Mûsã, amani imshukie, kikweli bila ya mtu wa kati (baina yao).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net