Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 162

An-Nisaa 4:162

النساء

لَّـٰكِنِ ٱلرَّٰسِخُونَ فِى ٱلْعِلْمِ مِنْهُمْ وَٱلْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ ۚ وَٱلْمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَ ۚ وَٱلْمُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلْمُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أُو۟لَـٰٓئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا

Maana

Lakini waliobobea katika elimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini yale yaliyoteremshwa juu yako, na yale yaliyoteremshwa kabla yako. Na wanaosimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, hao tutawapa malipo makubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini walio bobea katika ilimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini uliyo teremshiwa wewe, na yaliyo teremshwa kabla yako. Na wanao shika Swala, na wakatoa Zaka, na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho - hao tutawapa malipo makubwa. [162]

[162] Lakini walio bobea katika ilimu, yaani wataalamu kweli kweli, miongoni mwa Mayahudi, na Waumini katika umma wako, Ewe Nabii, wanasadiki wahyi ulio funuliwa wewe, na walio letewa Mitume wa kabla yako. Na wanao shika Swala baraabara, na wanatoa Zaka, na wanamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa na hisabu, hao Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kabisa kwa imani yao na ut'iifu wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini wale waliojikita katika elimu katika hukumu za Allah Mtukufu kati ya Mayahudi na wanaomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wanayaamini yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwako, ewe Mtume, nayo ni Qur’ani, na yale Aliyoyateremsha kwa Mitume kabla yako, kama Taurati na Injili, wanatekeleza Swala kwa nyakati zake, wanatoa Zaka za mali zao na wanamuamini Allah Mtukufu, kufufuliwa na malipo. Hao Allah Mtukufu Atawapa thawabu kubwa, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net